Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Abdulaziz Saleh bin Habtoor, mjumbe wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen, amelaani mashambulizi ya kikatili na yasiyo ya kibinadamu yanayofanywa na ndege za kivita za Saudi Arabia dhidi ya raia wasio na hatia katika majimbo ya Taiz, Sana'a na Sa'dah. Amesisitiza kuwa damu ya wananchi wa Yemen haitasahaulika wala kufutika kwa kupita muda, na kwamba utawala wa kihalifu wa Saudi Arabia utapata adhabu inayoustahili katika siku zijazo.
Kulaani mashambulizi ya anga ya Saudi Arabia
Abdulaziz Saleh bin Habtoor, mjumbe wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen, amelaani mashambulizi ya kikatili na yasiyo ya kibinadamu ya anga yanayofanywa na Saudi Arabia, ambayo ni adui wa wananchi wa Yemen, dhidi ya raia wasio na hatia katika majimbo ya Taiz, Sana'a na Sa'dah.
Mauaji katika soko la wananchi la Al-Wazi'iyyah na kukatika mawasiliano huko Sa'dah
Katika maelezo yake, Bin Habtoor alisema kuwa; ndege za kivita za Saudi Arabia zililenga soko la wananchi katika wilaya ya Al-Wazi'iyyah, mkoani Taiz, shambulizi lililosababisha kuuawa na kujeruhiwa makumi ya raia.
Aliongeza kuwa mashambulizi hayo pia yalilenga minara ya mawasiliano na simu katika mkoa wa Sa'dah, na kusababisha kukatika huduma za simu na intaneti kwa wananchi.
Kubomolewa nyumba za wananchi katika eneo la Bani Hashish
Aidha, alisema kuwa ndege za kivita za Saudi Arabia pia ziliharibu nyumba kadhaa za wananchi katika eneo la Bani Hashish, mkoani Sana'a, jambo lililosababisha kuuawa na kujeruhiwa makumi ya raia.
Uhalifu wa kivita na ahadi ya kulipiza kisasi
Mjumbe huyo wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen alisisitiza kuwa vitendo hivyo vya kikatili vya Saudi Arabia vinastahili kulaaniwa kwa maneno makali zaidi. Alieleza kuwa vitendo hivyo ni uhalifu wa kivita ambao hautafutika wala kusahaulika kwa kupita muda wowote, na kwamba utawala wa kihalifu wa Saudi Arabia utaonja adhabu ya matendo yake katika siku zijazo.
Pongezi kwa mafanikio ya kijeshi ya jeshi la Yemen
Mwisho wa maelezo yake, Bin Habtoor alisifu nafasi na mafanikio ya kijeshi ya jeshi la Yemen katika kushambulia kwa mabomu viwanja vya ndege vya Saudi Arabia, pamoja na maeneo yanayohusishwa na kampuni za mafuta na gesi na maeneo mengine.
Maoni yako